Friday 28 November 2014

SHEIKH PONDA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA KUU


Mahakama Kuu ya Tanzania imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda baada ya kuona hana hatia dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self  iliyokuwa inamkabili.

Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema baada ya kupitia vifungu vyote mahakama imejiridhisha na kuona Sheikh Ponda hana hatia yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa rumande akisubiri kesi nyingine ya madai ya uchochezi,  Mkoani Morogoro inayomkabili.

Thursday 27 November 2014

MAITI ZA WALIOKUFA KWA EBOLA ZATUPWA HOVYO MTAANI


Wahudumu wa Afya nchini Sierra Leone waliopewa kazi ya kuzika maiti za wagonjwa waliokufa kwa ebola wameamua kuitupa miili hiyo mitaani kutokana na kulalamikia posho ndogo wanazolipwa na Serikali ya nchi hiyo.
Katika kitendo cha kushangaza waliamua kutupa miili 15 ya maiti hizo katika mitaa mbalimbali kwa lengo la kuelezea hisia zao za kuchoshwa na malipo madogo wakati wanafanya kazi kubwa.
Wafanyakazi hao waliripotiwa kukaa siku saba bila kulipwa fedha zao ambapo kwa wiki hulipwa dola100 ambazo walidai ni ndogo ukilinganisha na kazi waliyokua wakifanya kudai inahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa.
Nyongeza ya fedha hizo walizokua wakitaka ni kwa ajili ya kufidia kazi wanazofanya kwa sababu hufanya katika mazingira magumu ya kuzika wagonjwa wa Ebola ambao huambikizwa kwa njia ya kugusana.
Kituo cha kitaifa kinachosimamia ugonjwa wa Ebola nchini humo kilitangaza rasmi kuwa wafanyakazi wote walioshiriki katika mgomo huo watafukuzwa kazi.

EMERSON AANZA MAZOEZI YANGA


Emerson de Oliveira Neves Roque  – mbrazil ambaye ameletwa nchini kuja kufanya majaribio na endapo ikifuzu basi ndio itachukua nafasi ya mbrazil aliyeondoka Jaja.Jana jioni mchezaji huyo huyo aliwasili na leo hii mchezaji huyo ameanza mazoezi mepesi asubuhi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola kufuatia kusaifri kwa zaidi ya masaa 11 kutoka jijini Rio de Janeiro.

Kiungo mbarazil Emerson de Oliveira a(wa pili kutoka kulia) akiwa mazoezini leo asubuhi katika uwnaja wa shule ya sekondari Loyola, wengine ni Kizza, Javu na Coutinho
Emerson ameungana na wachezaji wengine wa Young Africans katika mazoezi ya leo asubuhi ikiwa ni siku yake ya kwanza katika ardhi ya Tanzania na kufanya mazoezi mepesi mepesi chini ya kocha msaidizi Leonardo Neiva kuijiweka fit na kutoa uchovu safari.
Kiungo huyo mwenye umbo lililonyumbulika ambae alikuwa akichezea timu ya Bonsucesso FC iliyopo lii daraja la pili nchini Brazi katika jiji la Rio de Janeiro pia msimu uliopita alikua akicheza soka la kulipwa katika nchi ya Poland latika klabu ya Piotrkow Trybunalski FC.
Kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo amesema mchezaji huyo leo alikua na programu ya mazoezi mepesi tu kutokana na uchovu wa safari na kesho anatarajiwa kuendelea na mazoezi na wenzake kulingana na ratiba iliyopo.
Endapo Emerson atafanikiwa kulishawishi benchi la Ufundi kumsajili  basi moja kwa moja ataingia makubaliano na klabu ya Young Africans kwa ajili ya kuitumikia kwenye michuano ya kimataifa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia bara.

HAYA NDIO MAJIBU ALIYOYATOA Mh MIZENGO PINDA BUNGENI MAPEMA LEO ASUBUHI


Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

“…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata vilema…“– Mbowe.

"Tumeona mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.

"Baada ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio fedha za umma?“– Mbowe.

"Kwa uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.

Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…“

"Ningeweza nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

ESCROW NDO MPANGO WA MJINI



RUTI MPYAAAAAAAAA...
KITU CHA T/ESCROW KKOO NAULI 400 KAMA KAWA

MTATIRO: NCHI IMEOZA HADI ALTARENI

                              Askofu Kilaini

HII NI KAULI ALIYOITOA JULIUS MTATIRO BAADA YA VIONGOZI WA DINI KUWA KWENYE LIST YA WALIOPATA MGAWO WA MABILIONI YA ESCROW
Tunapokuwa na nchi iliyooza, viongozi wa dini wako mstari wa mbele kuchukua milungula na hela za rushwa zilizojaa damu na mateso ya kodi za wananchi.Ni aibu mno, sielewi hawa maaskofu wangu wanasimama kwenye altare kufanya nini...ni kufuru na aibu kwa mimi Mkatoliki na wakatoliki wote duniani.
Wakati Bunge linafukuza wezi, ni muhimu na Kanisa Katoliki lifukuze hawa maaskofu walafi na kuwapeleka mahakamani. Kisha kanisa lijivue ushenzi huu, lirejeshe pesa hizi kwa niaba ya watumishi hawa walafi wa fedha na mafisadi.
Shame on you beloved bishops, my bishops... 
#BishopMethodius #Kilaini & #BishopEusebius #Nzingilwa. 
#IPTL & #ESCROW #BringBackOurMoney.

SHILOLE TOTO LA KINYAMWEZI LATUA UBELGIJI....CHEKI MAFOTO YAKE HAPA ALIVYOPOKELEWA...










BREKI ZA NDEGE ZAGANDA BAADA YA KUPIGWA NA BARIDI KALI


Abiria waliokuwa wanafanya safari na shirika la ndege la Serbia walilazimika kushuka katika ndege hiyo na kuisukuma baada ya breki zake kuganda na kushindwa kuondoka.
Ndege hiyo ilikuwa inaanza kuruka kutoka katika mji wa Kirusi wa Igarka,lakini ilishindwa kusogea baada ya hali ya hewa kuwa -52C.
Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo idadi yao kubwa walikuwa wafanyakazi wa ndege hiyo waliombwa kutoa msaada wa dharura wa kuisukuma ndege hiyo kwa hofu ya kutowachelewesha endapo watasubiri msaada Zaidi.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Katekavia baada ya muda ilimudu kuendelea na safari zake na baadaye kutua salama katika mji wa Krasnoyarsk.kwa muujibu wa mashuhuda wa tukio hili kiwango cha baridikwa muujibu wa mashuhuda wa tukio hili ,wanaeleza kuwa kiwango cha baridi kilishuka hadi kufikia nyuzi joto 52, na kugandisha mfumo wa breki za ndege hiyo .
Mkuu wa kitengo cha huduma za ndege hiyo Oxana Gorbunova, anaeleza kwama abiria hawakulazimishwa kuisukuma ndege hiyo bali kwa hiyari waliamua kusaidia kuisukuma ,japokuwa kitendo hicho hakiruhusiwi kwakuwa kitendo hicho kinaweza kuathiri bodi ya nje ya ndege hiyo ,na wanasheria nao wanachunguza endapo uwanja wa ndege,shirika la ndege,wafanyakazi wa ndege ama abiria endapo wamevunja sheria za usalama wa anga.
Uwanja huo wa ndege unatumiwa na abiria takribani elfu moja kwa mwaka ,wengi wao hufanya kazi katika makampuni ya mafuta yanayomilikiwa na Urusi.
CHANZO:BBC