Tuesday 25 November 2014

JESHI LA NIGERIA MDEBWEDO,HUWAKIMBIA BOKO HARAM


Viongozi wa juu wa dini ya kiislam nchini Nigeria wameli shambulia jeshi nchi hiyo na pia kuwashutumu kuwa hukimbia mashambulio yanayofanywa na kundi la kigaidi la kiislam la Boko Haram.

Bodi hiyo inayoongozwa na Sultan wa Sokoto,imesema kwamba jeshi hilo limekuwa na tabia ya kutelekeza silaha zao kwa jeshi na kukimbialia mafichoni , na pindi mambo yanapotulia hurejea uraiani na kuwatishia raia.

Maelfu ya raia wa Nigeria wamekimbilia Niger kufuatia shambulio la hivi karibuni kutoka kwa kundi hilo la Boko Haram.

Waasi hao hujifanya kuwa ni wafanyabiashara walobebelea maboksi yenye bidhaa sokoni katika mji wa Damasak mji ulio Kaskazini mwa nchi ya Nigeria.

Lakini imebainika kwamba boksi hizo huwa zimesheheni bunduki,ambazo hutumika kushambulia raia wasio na hatia.

MDOMO WAMPONZA MWANAMKE,PAKISTANI


Mwanamke mmoja amehukumiwa adhabu ya kifo nchini Pakistan kwa kosa la kufuru, naye amekwisha kukata rufaa katika mahakama kuu nchini humo,hukumu hii imekuja miaka minne nyuma baada ya kukutwa na hatia kwa kumtukana mtume Muhammad Swalalahu ale wa Salaam.

Wakiili wa Asia Bibi anaamini kwamba rufaa yao itafanikiwa na mashauri yatakuwa baada ya mwaka mmoja.

Asia anashutumiwa kwa kufuru na kikundi kimoja cha wanawake wa kiislam kwa madai ya bibi huyo kutokuwa tayari kugusa birika la maji baada ya wanawake hao kulishika kwa madai ya imani yake.

Pakistani katika sheria zake haina kawaida ya kunyonga raia wake kwa kosa la kufuru lakini mashtaka, adhabu na vifungo vimekuwepo mara kwa mara kwa makosa ya kuutusi uislam.

WAZIRI WA ULINZI WA MAREKANI,CHURK HAGEL,HAJIULIZI


Habari kutoka Pentagon zinasema kuwa, Hagel amekuwa akifanya mazungumzo na Rais Barack Obama tangu mwezi Oktoba kuhusu kujiuzulu kwake. Duru za ndani ya Pentagon zinasema Rais Obama alimuomba Hagel kujiuzulu baada ya chama chake cha Democrats kushindwa vibaya kwenye uchaguzi mdogo uliokamilika majuzi. Imedaiwa kuwa, Hagel ameshindwa kukabiliana na changamoto za hivi karibuni zinazolikabili jeshi la Marekani ikiwemo kadhia ya Afghanistan na oparesheni dhidi ya kundi la kigaidi la ISIL. Hagel ataendelea kushikilia wadhifa wake hadi papatikane shaksia mwingine wa kujaza nafasi hiyo.

Jack Reed, Seneta wa jimbo la Rhode Island ni miongoni mwa wale wanaopigiwa upatu wa kuchukua nafasi hiyo.

Sunday 23 November 2014

RADI YAUA 6 SONGEA

Watu 6 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa wilayani Songea mkoani Ruvuma baada ya kupigwa na radi kufuati mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Jumamosi..

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela amesema kuwa maafa hayo yalitokea majira ya saa mbili usiku wakati watu hao wakila chakula cha usiku kwenye mgahawa wa chuo cha kilimo na mifugo cha Liti Madaba Songea

Kamanda huyo ameongeza kuwa mvua kubwa ilinyesha majira ya saa moja na nusu hadi saa mbili na baadaye ikapiga radi na kuua watu sita na kujeruhi watu wawili.

Amewataja waliopoteza maisha kwa kupigwa na radi kuwa ni Chesco Luoga mwanafunzi wa chuo cha Liti Madaba na mkazi wa Ludewa, Lucas Mabula mwanafunzi wa chuo hicho na mkazi wa Magu mkoani Mwanza, Eva Chapile muhudumu wa mgahawa wa chuo hicho, Osiana Antoni mhudumu wa Mgahawa wa chuo hicho, Justine Ngonyani mkulima na mkazi wa madaba Songea na Edwini Fungo mkulima na mkazi wa Madaba Songea.

Amewataja majeruhi kuwa ni Beatrice Mhagama mwanafunzi wa chuo cha Kilimo na mifugo Liti Madaba na mkazi wa Peramiho Songea na Leokadia Fusi muhudumu wa mgahawa wa chuo hicho na kwamba miili ya marehemu na majeruhi wako katika kituo cha afya Madaba.

Kutokana na tukio hilo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu na Mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Joseph Mkirikiti wameenda eneo la tukio Madaba Songea na kueleza kusikitishwa na tukio hilo na kusema huo ni msiba mzito kwa mkoa wa Ruvuma.

Saturday 22 November 2014

BONDIA MTANZANIA NA MANNY PACQUAIO KUPANDA ULINGONI USIKU WA LEO


BONDIA wa Tanzania wa Ngumi za Kulipwa, Fadhil Majia usiku wa leo Jumamosi anatarajia kupanda ulingoni nchini China kuzichapa na Jerwin Ancajas katika pambano la utangulizi la kimataifa kati ya Mfilipino, Manny Pacquaio na Cris Ageiri.

Tanzania ndiyo nchi pekee kutoka Afrika yenye bondia katika pambano hilo kubwa duniani litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Cotai Arena, Venetian Resort, Macao humo.Akizungumza na Championi Jumamosi, Katibu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Anthoy Rutta, alisema Manny Pacquiao na Fadhili Majia wamepima uzito jana usiku tayari kwa pambano hilo.

“Mabondia wote watakaocheza kwenye pambano la Jumamosi (leo) wamepima uzito na afya zao usiku wa jana akiwemo Manny Pacquaio na Mtanzania Fadhil Majia tayari kwa kazi hiyo.

“Majia ndiye atakuwa bondia wa kwanza kucheza pambano la utangulizi na Jerwin Ancajas, pia ni bondia pekee anayetokea barani Afrika, hivyo tunamtakia kila la kheri katika pambano lake,” alisema Rutta.  
Source: Gazeti la Champion Jumamosi

CHANONGO AGOMA KUICHEZEA SIMBA,KISIGA AULILIA UONGOZI


Kiungo wa Simba, Shaban Kisiga ameupigia magoti uongozi wa timu hiyo akiomba umrudishe kwenye timu huku kiungo mshambuliaji, Haruna Chanongo akigoma kuichezea timu hiyo.

Hivi karibuni uongozi wa Simba uliwasimamisha wachezaji watatu, Amri Kiemba, Kisiga na Chanongo kufuatia madai ya utovu wa nidhamu na kucheza chini ya kiwango kwenye mechi dhidi ya Tanzania Prisons katika matokeo ya bao 1-1.

Aidha, kwa upande wa Kiemba, uongozi wa Simba upo katika mazungumzo ya kumuuza mchezaji huyo kwa Azam FC ambapo wanataka walipwe kiasi cha shilingi milioni 15 badala ya milioni 10 wanayoitaka wao.

Kikizungumza na Championi Jumamosi, chanzo cha kuaminika kutoka Simba kimefunguka kuwa, Kisiga ameamua kuuomba msamaha uongozi wa klabu hiyo kufuatia kosa la utovu wa nidhamu alioufanya ambapo tayari amesharudishwa kundini kujiunga na wenzake.

Kilieleza kuwa, kwa upande wa Chanongo, amegoma na hataki kuisikia Simba wala kuichezea tena na badala yake anahitaji aachwe, hivyo kuwapa wakati mgumu viongozi wa timu hiyo.

“Kuhusu Kisiga ishu yake iliisha zamani, aliomba msamaha kwa utovu wa nidhamu alioufanya kwa hiyo ataungana na wenzake mara baada ya kikosi kuanza mazoezi.

“Kwa upande wa Chanongo suala lake linaonekana kuwa gumu, mwenyewe hataki kuichezea Simba, haijajulikana nini hatma yake kwani kuna baadhi ya viongozi wanapendekeza arudishwe Simba B lakini bado hatujaafiki suala lake,” kilisema chanzo hicho.
SOURCE: GPL

MAGAZETI YA UDAKU NA MICHEZO LEO HII JUMAMOSI NOVEMBA 22


















MAGAZETI YA BONGO LEO HII JUMAMOSI NOVEMBA 22