Thursday 27 November 2014

MAMA MJAMZITO AMPIGA TAFU MUMEWE KUBAKA BINTI WA MIAKA 7


Mwanamke mmoja nchini China ambaye ni mjamzito amehukumiwa kifungo cha maisha huku mume wake akihukumiwa adhabu ya kifo baada ya kushirikiana kumbaka na kisha kumuua msichana wa miaka17.
Mwanamke huyo ambaye anajulikana kwa jina la Tan Beibei alifanya kitendo hicho baada ya msichana huyo kumsaidia alipoanguka barabarani ambapo alimpeleka hadi nyumbani kwake na badala ya kumshukuru waliamua kumfanyia kitendo hicho cha akishirikiana na mumewe kisha kumuua na kuamua kumzika.
Mahakama ya Heillojiang ya nchini humo imesema kuwa imewafungulia mashtaka ya kuua,kubaka pamoja na kushambulia baada ya mwanamke huyo kujifanya ni mgonjwa na kushirikiana na mumewe kumfanyia binti huyo kitendo hicho cha kudhalilisha kisa wivu kwa madai alikua akitembea na mumewe.
Mahakama ya juu ilikataa kuwapunguzia adhabu wawili hao baada ya kukata rufaa kwa madai kesi hiyo ni kubwa na haina dhamana yoyote.
Kwa mujibu wa mashuhuda msichana huyo aliyejulikana kwa jina la Hu alikua akipita barabarani ndipo mama huyo alipomwomba msaada wa kumpeleka nyumbani kwake baada ya kuanguka na msichana huyo kutii lakini alipofika alikutana na maswaiba hayo.
Inaelezwa kuwa baada ya kufika mume wa mwanamke huyo alimpa msichana huyo maziwa ya mtindi na baadaye kuanza kumfanya kitendo hicho lakini hata hivyo hawakufanikiwa kwani binti huyo aliweza kuwazidi nguvu na walipoona imeshindikana walichukua blanketi na kumziba nalo usoni hadi alipofariki dunia na kuamua kumzika.
Katika utetezi wa mwanamke huyo mahakamani hapo alisema aliamua kufanya kitendo hicho kwa sababu binti huyo alikua akitembea na mume wake.
Historia inaonyesha wawili hao walishawahi kuwa na kesi mbalimbali kiwemo ya kutaka kumbaka rafiki wa mtoto wao wa kike ambaye alikua akisoma naye darasa moja.

BAADA YA KIM KARDASHIAN SASA NI ZAMU YA WIZ KHALIFA KAJIFOTOA MTUPUUUUUUU AKIWA BAFUNI


Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Supastaa Kim Kadarshian kukaa kwenye vichwa vya habari vya mitandao mbalimbali kutokana na picha zake zikimuonyesha akiwa tupu kuzagaa kwenye mitandao, staa mwingine tena huenda akaingia kwenye list ya #BreaktheInternet.
Kwenye ukurasa wa Rapa Wiz Khalifa ameweka picha inayomwonyesha akijimwagia maji kichwani huku akiwa mtupu ndani ya bafu.
Bado haijafahamika kama amefanya hivyo kama njia ya kuyatangaza maji hayo au ana maana ipi.

KASHFA YA MISS TANZANIA 2014,UTATA MPYAAAAAAA WAIBUKA


Hatima ya kashfa ya kudanganya umri inayomkabili aliyekuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2014, Sitti Mtemvu bado ipo kizani baada ya polisi kuikana kauli ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

Rita, kwa upande wao ilieleza wiki moja iliyopita kuwa imekabidhi polisi vielelezo kuhusu uchunguzi wa kashfa hiyo kwa lengo la kuchukua hatua.

Juzi, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikana kupokea taarifa za vielelezo hivyo vilivyotumiwa kuombea cheti cha kuzaliwa cha Sitti Mtemvu.

Wiki mbili zilizopita, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ilijivua lawama katika kashfa hiyo na kuiachia Rita.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Kova alisema, “Jeshi la Polisi halijapokea vielelezo vyovyote kutoka Rita, wamepeleka wapi? Iwapo waliviwasilisha katika kituo chochote cha polisi watoe taarifa iliyo sahihi, iwapo vielelezo hivyo vitatufikia tutachukua hatua stahiki,” alisema Kova.

Kwa upande wao, Rita waliahidi kuwasilisha vielelezo hivyo wiki hii na kwamba vilicheleweshwa kutokana na kukamilisha upekuzi wa taarifa za kuombea cheti pamoja na cheti cha awali kilichokuwa kikitumiwa na Sitti Mtemvu.

Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Rita, Emmy Harrison alisema jana kuwa idara yake imekamilisha taratibu zote zinazotakiwa na vielelezo hivyo vitakabidhiwa rasmi polisi.

“Haya ni masuala ya kisheria, hivyo sisi tumeshakamilisha kile tulichotakiwa kukifanya na mchakato huu bado unaendelea, tupo katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kuripoti polisi, wiki hii vielelezo vya Sitti vitapelekwa kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema Harrison.
CHANZO: MWANANCHI

MRITHI WA JAJA HUYOOOOOOOOO KASHATUA.......



Nyota mpya wa Klabu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam, anayekuja kufanya majaribio ya kuziba nafasi ya Mbrazil mwenzake Genlson Santos 'Jaja', Emerson De Oliveria Neves Rouqe akitoa ishara ya dole mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa Yanga. 
Rouque aliwasili na Kocha mkuu wa Yanga, Marcio Maximo pamoja na Nyota mwingine kutoka Brazili Andrew Coutinho.

ICHEKI SURA YA YULE BEKI TATU WA UGANDA BAADA YA KUPOKEA KICHAPO HEVI



Huu ndio muonekano wa yule msichana wa kazi za ndani aliye tenda unyama wa kutaka kumuua mtoto wa bosi wake atimaye naye amepokea kipigo takatifu cha nusu kufa kutoka kwa wazazi wa uyo mtoto hii ni moja ya picha zilizo vuja ambazo wazazi wa mtoto family iyo walizificha.

VYUO VIKUU TANZANIA HOVYO KABISA....VYAIAIBISHA NCHI...


Vyuo vikuu vitatu vya Tanzania ambavyo vilishiriki katika mashindano ya mjadala wa Afrika kuhusu Sheria za kimataifa za haki za kibinaadamu yalioandaliwa na kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC vimeshindwa kufika katika raundi ya mwisho.

Badala yake vyuo hivyo viliondolewa katika raundi za mapema ambapo mataifa manane ya Afrika yalishiriki.

ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa mjini Arusha.

Kulingana na gazeti la the Citizen nchini Tanzania, vyuo vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo kikuu cha Zanzibar.

Katika raundi ya mwisho ya mashindano hayo yaliofanyika mwishoni mwa wiki katika mahakama maalum ya kimataifa inayochunguza mauaji ya kimbari nchini Rwanda ICTR mjini Arusha,chuo cha Strathmore University kutoka Kenya kiliibuka mshindi na kufuatiwa na chuo cha Christian University kutoka Uganda huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka Zimbabwe kikiibuka mshindi wa spika bora.

Raundi ya mwisho ya mjadala huo ilisimamiwa na jaji wa mahakama hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji wa mahakama ya haki katika Afrika mashariki Fanstin Ntezilyayo,John Joseph Wamwara na Mutsa mangezi kutoka ICRC.

Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi kwa washindi aliyapongeza mashindano hayo kama kifaa cha kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya sheria na kwamba itasaidia kuimarisha maono yao katika siku za usoni.

UBAGUZI WA RANGI WAKITA MIZIZI MAREKANI....WATU WEUSI WAWEKWA GEREZANI,WAHUKUMIWA KIFO NA WENGINE WAPIGWA RISASI NA POLISI


Mkuu wa Haki za Binaadamu Katika Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu 'ubaguzi uliokita mizizi' na idadi kubwa kupita kiasi ya Wamarekani weusi au wenye asili ya Afrika ambao wanauawa na polisi nchini Marekani.

Zeid Ra’ad Al Hussein Kamishna wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa kuna idadi kubwa kupita kiasi ya Wamarekani weusi wanaoshikiliwa gerezani na wanaosubiri kutekelezwa hukumu za kifo dhidi yao.

Matamshi hayo yametolewa kufuatia ghasia kubwa zilizoibuka baada ya jopo la mahakama huko Missouri, Marekani kumuondoa hatiani afisa mzungu wa kikosi cha polisi ambaye alimpiga risasi na kumuua kijana Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Michael Brown, katika mji wa Ferguson. Ghasia zimeripotiwa katika miji zaidi ya 90 kote Marekani ambapo waandamanaji wanalalamikia ukandamizaji na ubaguzi wa wazi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika katika mfumo wa utawala nchini Marekani. Gavana wa Jimbo la Missouri, Jay Nixon, ameagiza wanajeshi wengine 2,200 wa Gadi ya Taifa kupelekwa Ferguson kukabiliana na waandamanaji wenye hasira.

MTI ULIOINUKA BAADA YA KUANGUKA MIAKA 3 ILIYOPITA WAENDELEA KUFANYA MAAJABU


Mti huo umeinuka siku ya Oktoba 15 mwaka huu, ambapo Katibu tawala wa Wilaya ya Uyuwi amesema;
 “…kwa mazingira tunayoyaona hapa tukio ni kweli limetokea sasa ni kwa nguvu zipi kwa uwezo wa Mungu au nguvu za giza hili nadhani kwa sasa litakuwa hatuwezi kulitolea taarifa ,lakini cha msingi eneo hili tulitunze kwa matumizi ya kumbumbuku ya vizazi vyetu na pamoja na wengine watakaotoka nje ya eneo hili, ambao watataka kuja kuona maajabu ya Mwenyezi Mungu tofauti na kule Mfuto ulipoinuka tu siku ya pili yake tukakuta kila kitu hakuna, kwa hiyo nilikuwa napenda niwapongeze Wanakijiji kwa kulinda Mti huu…”

Shuhuda wa kwanza kuzungumzia tukio hilo amesema; “… Haya magome ya mzizi yakichimbwa, yakisagwa mtoto akiwa anaumwa Degedege wakimvutisha ile hali ya mchango inashuka hata kama unaumwa kipanda uso, hata kama unaumwa kichwa cha kawaida…”

Mwanakijiji mwingine amesema; “…Huu Mti kama mbwa wako sio mkali unachimba mizizi unakoboa magome unatwanga ule unga wake unamnusisha kwenye pua anakuwa mkali sana…“

Mtu mwingine amesema; “Kama kuna Mtu ambaye pengine kashaishiwa pengine fahamu wanajaribu kumuwekea puani na mara anapiga chafya…”