Saturday 22 November 2014

JOKATE NA GAETANO KUFANYA KIPINDI KIPYA NDANI YA M Net EAST AFRICA


Mbunifu wa mitindo na muigizaji wa filamu nchini, mrembo Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na mshiriki maarufu wa Big Brother Africa, Mganda Gaetano Kagwa wameteuliwa kuendesha kipindi kipya cha Maisha kijulikanacho kwa jina la “Beat the Challenge” kupitia M-Net East Africa.
Kipindi kitashindanisha familia mbalimbali katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda na mshindi atapewa gari jipya kabisa kutoka kwa waandaaji.  Katika mashindano hayo, kila  familia inatakiwa kuwa na watu wanne ambao ni Baba, Mama na watoto wawili wenye umri kati ya miaka 12 na 17.
Familia hizo zitashinda katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazowasilishwa na waandaaji na kila familia itakuwa na jukumu la kutatua hizo changamoto kwa kutumia nguvu kuliko ufahamu wa akili.
Akizungumza jana Jokate alisema kuwa amejisikia faraja kubwa kupewa nafasi hiyo ambayo itampa uzoefu zaidi katika fani ya utangazaji na kujipanua kimawazo.
Jokate ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kwa kuzidi kuongeza wigo wa mawasiliano kwani hii si mara yake ya kwanza kuendesha vipindi katika televisheni baada ya kutamba katika kipindi cha Chaneli O.
“Kama nilivyosema, nataka kuishi kwa kutegemea vipaji vyangu na wala si vinginevyo, nimeanza katika urembo, nikaja katika ubinifu na uanaminitindo, MC, muigizaji wa filamu na sasa mtangazaji, kote huko nimefanikiwa, ni faraja kubwa kwangu,” alisema Jokate.
Alisema kuwa anashukuru kuona kuwa filamu yake ya Mikono Salama kwa sasa inatamba sana na inamuongezea sifa kubwa katika fani hiyo. “Hata kidoti Fashion nayo inatamba, hivyo kwa nashukuru Mungu kwa kuniwezesha,” alisema.
Kwa upande wa Tanzania, utafutaji wa washiriki utafanyika Jumamosi Novemba 22), New Africa Hotel, wakati Uganda watafanyia kwenye hotel ya Silver Springs, Kampala na Kenya kwenye studio za Supersport zilizopo katika Barabara ya Jamhuri.
Kipindi cha kwanza kitarushwa Desemba 13 kupitia chaneli ya Maisha Magic 161 kuanzia saa 2.30 usiku kwa mujibu wa Jokate.

MISS SINZA APIGA TENA PICHA ZA UCHI


Miss Sinza 2001 na aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid ameonesha kuwa ni sikio la kufa baada ya kupiga picha za utupu kwa mara nyingine.



Picha hizo zilizotapakaa kwenye mitandao mbalimbali zimewashangaza watu ambapo Husna anaonekana akiwa kama alivyozaliwa huku akiwa katika mapozi tofauti hali inayoonesha kwamba alikuwa akipigwa picha hizo na mpenzi wake.

Kwa mujibu wa mdau ambaye aliziweka picha hizo kwenye mtandao wa Instagram, mwanadada huyo alipigwa picha hizo na mpenzi wake ambaye hakumtaja jina.Alisema mpenzi wake huyo alimuomba ampige picha ili awe anaziangalia kila wakati kwani anampenda sana ambapo Husna alikubali kupigwa picha hizo lakini matokeo yake zikazagaa mitandaoni.

KASHFA YA IPTL & ESCROW YAPELEKEA NIMROD MKONO KULISHWA SUMU UINGEREZA

Mh Nimrod Mkono (Mb) amekoswakoswa kuuawa nchini Uingereza alikokuwa amekwenda kikazi. Aliwekewa sumu ambayo ilipaswa iharibu kabisa figo zake ndani ya saa 72. Uongozi wa bunge umethibitisha na ripoti ya madaktari wa London inaonesha hivyo.

Mkono mwenyewe anasema alionywa kuwa usalama wake uko mashakani na akatakiwa asifikie katika hoteli ambayo ujumbe wa viongozi wa Tanzania utafikia.
Mkono anasema alipofika London aliamua kwenda katika nyumba yake binafsi, lakini baadaye alianza kutoka jasho, kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu kwa saa 6.

Ikumbukwe kuwa Mkono na kampuni yake ya Mkono & Advocates ndiyo iliyokuwa inatetea upande wa TANESCO na Serikali katika kesi dhidi ya IPTL.
Inasemekana Mkono anatafutwa kuuawa kwa sababu inaonekana ana taarifa nyingi mno kuhusu sakata la IPTL na ESCROW, na serikali inamtuhumu kuwa yeye ndiye aliyevujisha nyaraka zote hadi umma wa watanzania kugundua kuwa zaidi ya bilioni 321 mali ya umma zimeibiwa katika sakata hilo.
CHANZO: GAZETI LA THE CITIZEN

POLISI ALIYEMUUA MWANAFUNZI CHUO KIKUU JIJINI MBEYA APEWA HUKUMU YA KIFO


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa polisi wa upelelezi, Maduhu, F 5842, aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Daniel Mwakyusa.

Aidha, mahakama hiyo imewaachia huru washitakiwa wengine wawili wa kesi hiyo, polisi wa upelelezi, Shaaban, F 7769, na polisi wa kike mpelelezi, Neema, F 6545, baada ya kuwakuta hawana hatia.

Hukumu hiyo ya kesi namba 16 ya mwaka 2013, ilitolewa jana mjini hapa na Jaji Rose Temba, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.

Awali, ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali, Archiles Mulisa akisaidiwa na Catherine Paul kuwa washitakiwa walifanya mauaji ya kukusudia Februari 14 mwaka 2012 kinyume cha Kifungu Namba 196 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa Marejeo mwaka 2002.

Mulisa alidai washitakiwa hao kwa pamoja walihusika na mauaji ya Daniel Mwakyusa baada ya kumpiga kwa kutumia silaha inayodhaniwa kuwa ni bunduki, nje ya ukumbi wa starehe wa Universal uliopo Uyole jijini Mbeya.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo, Jaji Temba alisema anawaachia huru mshitakiwa namba mbili, Shaaban ambaye alikuwa dereva wa gari ya polisi kwa kuwa ushahidi uliotolewa, unadhihirisha kuwa alibaki ndani ya gari akimsubiri mshitakiwa namba moja aliyeshuka na kuingia kwenye ukumbi wa Universal.

Kwa upande wa mshitakiwa namba tatu, Neema, Jaji Temba alisema aliridhishwa na mshitakiwa huyo kutohusika na mauaji kwa kuwa siku ya tukio alikuwa akijisikia vibaya, hivyo alilazimika kubaki na dereva kwenye gari.

Jaji Temba alisema mshitakiwa namba moja, Maduhu, anahusika moja kwa moja na mauaji hayo, kutokana na ushahidi wa kimazingira, kwani yeye ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kuondoka na Daniel Mwakyusa eneo la tukio na kumpeleka kwenye gari.

Alisema sababu ya pili, ushahidi ulionesha kuwa silaha yake pekee ndiyo iliyotumika, tofauti na za askari wengine kwa kuwa risasi tatu zilionekana kupungua kati ya zile alizokabidhiwa sambamba na ushahidi wa maganda matatu ya risasi, yaliyookotwa eneo la tukio.

Jaji Temba alisema sababu ya tatu ni kuwa ushahidi uliotolewa, unaonesha kuwa mshitakiwa huyo alikuwa wa mwisho kurejesha silaha, hivyo kuhusishwa moja kwa moja na mauaji hayo.

Alisema kutokana na sababu hizo, mahakama inamtia hatiani kwa kuua kwa kukusudia, hivyo mshitakiwa Maduhu, amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Awali, ilidaiwa kuwa siku ya tukio ilikuwa Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day), ambapo mtuhumiwa akiwa doria na askari wenzie, alimkuta Daniel Mwakyusa akiwa kwenye eneo la starehe na mwanamke anayesadikiwa kuwa alikuwa pia na mahusiano na askari huyo.

MFUMO MPYA WHATSAPP WAVUNJA NDOA ILIYODUMU MIAKA 2


Wiki chache baada ya WhatsApp kutambulisha mfumo mpya ambapo iwapo unamtumia message mtu inakuonyesha alama ya tick mbili za kijani na pia inaonyesha muda ambao mtu uliyemtumia message hiyo ameisoma, tayari kuna ndoa ambayo imeingia matatizoni kutokana na hilo.
Mwanaume mmoja Saudi Arabia ametoa talaka kwa mkewe kutokana na kitendo cha mwanamke huyo kutokujibu message aliyomtumia WhatsApp.
Mwanaume huyo amesema kitendo kilichomkasirisha zaidi ni pale aliporudi nyumbani na kumkuta mke wake akiwa busy anachat na marafiki zake kupitia mtandao huo wakati message aliyomtumia yeye hakuijibu.

Jamaa huyo ameona kama kitendo hicho ni dharau kubwa na hakuwa tayari kuendelea na ndoa hiyo ambayo imedumu kwa miaka miwili tangu ifungwe.

ARSENAL YAWAKOSA MESSI NA PIQUE


Kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kuwa kilabu hiyo ilijaribu kumsajili nyota wa kilabu ya barcelona Lionel Messi kama mpango wa kutaka kuwanyakua wachezaji watatu wachanga wa kilabu hiyo.

Messi alikuwa na miaka 15 wakati huo na mwenzake Gerrad Pique pamoja na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Cess fabregas.

Wenger:''Tulitaka kumchukua Fabregas,Messi na Pique,lakini tukafanikiwa kumpata Fabregas pekee''.

Fabregas aliichezea kilabu ya Arsenal kwa miaka minane kabla ya kurudi Barcelona ,huku Pique akijiunga na Manchester United mwaka 2004.


Messi mwenye umri wa miaka 27,ameichezea timu ya Barcelona kwa muda wote na kuisadia kushinda mataji sita ya La liga pamoja na kombe la vilabu bingwa mara tatu baada ya mpango wa kujiunga na Arsenal kugonga mwamba.

Hatahivyo ,Wenger amepinga madai kwamba mpango huo ulifeli kutokana na makaazi ya Messi na familia yake. Mchezaji huyo wa timu ya Argentina pia angelazimika kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza.

Wenger aliongezea:''Nadhani Messi mwenyewe hakutaka kujiunga nasi''.

BAADA YA KUKATALIWA KUPANDA NDEGE KWENDA INDIA KWA MATIBABU,KIJANA WA KITANZANIA AFARIKI DUNIA


Sande Jacob Mremi (pichani) amefariki Siku chache baada ya kukosa usafiri wa ndege ambapo alitakiwa kwenda nje ya nchi kupata matibabu.
Kituo cha ITV kiliripoti kuhusu habari za kijana huyo kuumwa na kutokana na kusumbuliwa tatizo la uzito mkubwa nakushindwa kupata Ndege ya kumsafirisha kwenda kwenye matibabu India kijana huyo amefariki Dunia.
Ndugu wa kijana huyo walilalamika kutoridhishwa na baadhi ya Mashirika ya Ndege kwa kushindwa kuwasaidia kumsafirisha ndugu yao.
Katika mahojiano na ITV mama wa mtu huyo amesema; “..yaani kwa kweli mashirika ya Ndege hayakuweza kutufanyia haki kwa kweli, wametunyanyasa kwa sababu tulipokuwa tunapeleka maombi tunataka kumsafirisha mtoto wetu ilikuwa wao watusaidie na kutupa maelekezo tunatakiwa tufanye nini na nini, lakini baada ya kuona tunakosa msaada ndio tukaamua kuja ITV ili watusaidie, kwa hiyo yeye mwenyewe akaanza kupata presha kwa sababu presha alikuwa hana mpaka anapanga kusafiri alikuwa hana presha nilimpima vipimo vyote alikuwa hana tatizo lolote…”
Dada wa marehemu amesema; “..Ethiopia walitusaidia kwa kweli mpaka hatua ya mwisho na Jumapili kama Mungu angemuweka hai Ethiopia wangemsafirisha, na mashirika ya Ndege mengine yalitakiwa yatuelekeze hivi, lakini sasa kutokana na ile hali mara leo kapelekwa kesho anarudishwa mdogo wangu kesho kutwa kapelekwa amerudishwa mdogo wangu, msongo wa mawazo umemkaa rohoni anashindwa kuongea maskini ya Mungu, mawazo paka yamemfanya mdogo wangu alikuwa hana presha paka presha imekuja paka mdogo wangu anafariki.

Baba wa Sande amesema; “…wakatumia sheria ya pili ya kunihusisha mimi wakaniambia bwana kumbe mtu huyu ni mkubwa sana tunatakiwa tuvunje viti tumbebe, nikawauliza nikulipeni bei gani? wakaniambia tulipe dola elfu saba mia tano na thelathini na nne, na mara ya kwanza tulilipa dola elfu sita miambili ishirini…”
Bado haijafahamika kama Shirika hilo la ndege litarudisha hela ambayo ililipwa na watu hao kwa ajili ya kumsafirisha ndugu yao.

KAIMU RAIS WA ZAMBIA ATIMULIWA CHAMANI


Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu wa katiba.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho.

''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya chama,'' amesema Malozo Sichone.

Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi utakapofanyika tarehe 20 Januari.

Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana.