Monday, 2 February 2015

GARETH BALE AONJA MACHUNGU YA MASHABIKI WA REAL MADRID KWA TABIA YAKE YA UCHOYO WA PASI..

 
Gareth Bale amekutana tena na adha za mashabiki wa Real Madrid baada ya kuzomewa na wanazi hao kwa kumnyima pasi mchezaji mwenzake.
Hata hivyo Bale aliwajibu kishujaa kwa kutoa pande zuri kwa Karim Benzema lililozaa moja ya magoli katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Real Sociedad Jumamosi jioni.  


Kundi dogo la mashabiki wa Real Madrid miongoni mwa umati uliofurika Santiago Bernabeu lilikerwa na Bale pale alipopoteza nafasi ya wazi wakati alipobaki yeye na kipa Geronimo Ruilli.

Muda mfupi baadae mshambuliji huyo akamnyima nafasi ya kufunga James Rodriguez kwa kujaribu kufunga mwenyewe lakini mkwaju wake ukatoka nje.

No comments: