Irene Uwoya amesema ingawa Jaguar alishindwa kuja kuzungumza na wazazi wake kuhusu ndoa yao, bado wanawasiliana vizuri na kila kitu kipo sawa.
Akizungumza jana, Irene amesema mahusiano yake na Jaguar yapo japo hajafanya maamuzi ya kuolewa.
“Jaguar hakuja kuna vitu ambavyo vilitokea vikasababisha asije,” amesema mrembo huyo. “Kila siku naongea naye na uamuzi wake upo pale pale. Mimi mwenyewe bado sijafanya maamuzi ya kusema niolewe lakini akija ndo tutaongea kila kitu.”
Msanii anayedaiwa kuwa na utajiri mkubwa kuliko wasanii wengine nchini Kenya, Jaguar
Haya hivyo Irene amesema hawezi kuzungumzia ndoa yake na mcheza soka wa Rwanda, Ndikumana waliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Krish.
“Sasa kuhusu hilo nisingependa kuliongelea, mimi nadhani sijui hata nisemeje, sipendi kuongelea mambo yangu binafsi.”
No comments:
Post a Comment