Friday 23 January 2015

ZARI KUWA NA MIMBA,INA MAANA DIAMOND ALIFANYA MAPENZI BILA YA KINGA,JE WALIPIMA LINI NA WAMEJUANA KWA MUDA GANI?????


Takribani wiki nzima sasa mitandaoni kumejaa hii habari ya kuwa shemeji na wifi yetu Zari the boss lady yu mjamzito,ambapo muhusika wa ujauzito huo ni Diamond...Nimekuwa nikijiuliza mwenzenu,Ili mtu aweze pata ujauzito kwa njia ya kujamiiana basi ni lazima afanye mapenzi bila kutumia kinga ya aina yoyote ile hususani Condom.. 
Hivyo kama kweli Zari ana mimba hii ina maanisha walifanya mapenzi kavu kavu na hapa ndipo ninapojiuliza mimi mwenzenu ZARI NA DIAMOND WALISHAPIMA AFYA ZAO??? WAMEJUANA KWA MUDA GANI MPAKA WAFIKIE UAMUZI HUO WAKUTEMBEA PEKU PEKU????  

Thursday 22 January 2015

ZIFAHAMU CLUB KUMI TAJIRI BARANI ULAYA,REAL MADRID YAFUNIKA


Real Madrid imeibuka kama klabu tajiri zaidi ulaya kulingana na orodha iliyotolewa na Deloitte Football Rich kwa miaka kumi mfululizo.
Manchester United imetoka nafasi ya nne hadi ya pili katika orodha hio, kulingana na mapato ya msimu wa 2013 -2014
Bayern Munich, Barcelona na Paris St -Germain walifuatana kwa orodha hiyo kutoka nambari tatu.
Klabu za Uingereza, Machester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool wanafuatana kutoka nambari sita hadi tisa, wote wakionyesha dalili nzuri za kuongeza mapato .

MASKINI RACHEL,AFUATA NYAYO ZA RAY C NAE SASA ALISHWA UNGWA NA KUVUTISHWA BANGI


Kama ilivyotokea kwa msanii nyota wa kike wa bongo fleva, Rehema Chalamira 'Ray C' kuingizwa katika matumizi ya dawa ya kulevya na mtu ambaye alitokea kumwamini sana, ndivyo ilivyotokea sasa kwa msanii anayefuata nyendo zake, Winfrida Josephat 'Rachel' ambapo anadaiwa kuvutishwa unga bila kujua.... 

CSKA MOSCOW YAMUONGEZEA MUDA MBWANA SAMATTA,LIST YA TIMU ZINAZOMTAKA HII HAPA...

 Hatimaye nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta imeanza kung’ara katika anga ya kimataifa ya soka.Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba mshambuliaji huyo yupo kwenye majaribio katika klabu ya CSKA Moscow – moja ya klabu kubwa kabisa nchini Urusi ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo na kucheza katika michuano ya mabingwa wa ulaya. 

JOKATE AMFUNIKA LULU,MWENYEWE AFURAHIA

 Mwanamitindo na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo 

MWANAMITINDO na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo amekuwa tishio kwa msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa urembo na muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini. 

MASIKINI TAMBWE ASIMULIA ANAVYONYANYASIKA,YANGA YAKIMBILIA TFF KUSHTAKI


Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya manyanyaso anayoyapata.

KUFUATIA SAKATA LA ESCROW,WAZIRI MUHONGO,NGELEJA MWAMBALASWA WAJIUZURU NAFASI ZAO....


WENYEVITI wa Kamati za Kudumu za Bunge, waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, wamejiuzulu nyadhifa zao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Spika Anne Makinda aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi ndogo ya Bunge, waliotaka kujua hatima ya wenyeviti hao, kuwa hawapo tena katika nafasi zao baada ya kujiuzulu.

Wednesday 21 January 2015

DIAMOND NOMA,AWEKA APPLICATIONA YAKE MWENYEWE GOOGLE PLAY....


  

Star wa Muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz bado anazidi kuongeza wigo wa kutoboboa kimuziki hasa kwa soko la ki mataifa,kwani hivi sasa ameweza kuwa amefikia hatua ya kuwa ana miliki application yake mwenyewe ya google play.