Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania,Flora Mbasha, amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar-es-Salaam, akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe Emanuel Mbasha.
Flora amefungua kesi ya madai namba 64 ya mwaka huu kesi ambayo inasikilizwa na hakimu Maxi, Devota Kisoka.