Saturday 31 January 2015

ROBERT MUGABE ATEULIWA KUWA MWENYEKITIBWA UMOJA WA AFRIKA "AU"..

Rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe, ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika AU akichukua nafasi ya Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania.
  Mugabe mwenye umri wa miaka 90 ameteuliwa kwa kauli moja na Wajumbe katika mkutano wa AU unaoendelea kwa sasa mjini Addis Ababa-Ethiopia.

LEMA: NATAMANI KWENYE AMRI ZA MUNGU IONGEZWE YA 11,ISEMAYO "USIWE CCM"..


   
 Wabunge wameendelea kuchangia taarifa za Kamati za Hesabu za Serikali PAC na LAAC zinazoonesha ubadhilifu mkubwa wa fedha za umma. Hapa  chini nimekuwekea  michango  ya  baadhi  ya  Wabunge.

Lema: Haiwezekani kila siku tukija humu tunazungumzia wizi tu, inatakiwa tuzungumzie mipango ya maendeleo ya wananchi sio kila siku wizi wizi wizi unaosababishwa na CCM..

BABA AJIUA BAADA YA KUONA PICHA ZA UCHI ZA BINTI YAKE


                         

Wazazi wamekua na nafasi kubwa sana katika malezi ya watoto wao hata wakati  wanapokuwa watu wazima lakini baba huyu kutokana na upendo kwa mwanaye aliamua kujiua baada ya kuona picha za mtoto wake alizopiga akiwa mtupu katika jarida la Playboy....

Thursday 29 January 2015

HUYU NDIYE MTANGAZAJI MWENYE SHEPU KAMA KALIMATI TANZANIA

MTANGAZAJI wa kituo cha Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’, juzikati aliamua kutoa siri yake ya moyoni na kuweka wazi juu ya tabia yake ya kuachika na kupata mume mpya mara kwa mara.Aliweka bayana kwamba anaachika na kupata mwanaume mpya haraka kwa sababu ana shepu ya kalimati (aina ya andazi linalonona).  

SHILOLE AMTANDIKA MAKOFI NUH MZIWANDÀ AWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE....


      

Baada ya kuzuka tetesi kuwa alimdunda vibao mchumba wake Nuh Mziwanda, Shilole amelazimika kuomba radhi.
Shilole amewaomba radhi mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram kwa kupost picha akiwa na mpenzi wake huyo na kuandika:
“Huyu hapa mjanja wangu mimi, daah nimekamatika hapa, na naamini ni mwanaume sahihi kwangu maana hawezagi kurusha hata ngumi japo namchokozaga mie mjeuri tu, mnao muhandama mme wangu mmeshindwa, kugombana ni kawaida sana kwenye mapenzi na kama nliwaudhi mashabiki wangu mnisamehe mie nampenda mme wangu.” 

Wednesday 28 January 2015

GHANA YAICHAPA AFRICA KUSINI 2-1:YATINGA ROBO FAINALI AFCON

                             
Ghana ilitoka nyuma ikiwa kwenye hatari ya kuaga michuano na kutumia dakika 17 za mwisho kuilaza Afrika Kusini 2-1 na kutinga robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
Katika mchezo huo uliopigwa Jumanne, mabingwa hao wa mara nne, wakaonyeshwa mlango wa kuagia mashindano baada ya mkwaju mkali wa Mandla Masango kuipatia bao Afrika Kusini kunako dakika ya 17.
Lakini Ghana wakafanikiwa kugeuza matokeo katika kipindi cha pili cha mtanange huo uliochezwa kwenye dimba la Mongomo Stadium. 

CHELSEA YAICHAPA LIVERPOOL,YATINGA FAINALI CAPITAL ONE CUP


                     

Chelsea imeifunga Liverpool 1-0 na kutinga fainali ya Capital One Cup kwa jumla ya bao 2-1 kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita.
Hata hivyo mpira huo ilibidi uchezwe kwa dakika 120 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 za kawaida bila kufungana.
Dakika ya 4 tu ya dakika 30 za ‘Extra Time’ beki Branislav Ivanovic akaifungia Chelsea bao pekee baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya mpira wa adhabu uliopigwa na Willian.  

HII NDIO ORODHA YA PASSWORD ZILIZOVUJA ZAIDI NA ZILIZITUMIWA NA WEZI WENGI WA MITANDAO 2014,TAZAMA KAMA YAKO IPO..


Hivi karibuni tumesikia watu wengi wakiwemo wasanii wakilamika juu ya account zao pamoja na simu kuvamiwa na wezi wa mitandaoni, watafiti wanasema matumizi ya password dhaifu pia huchangia account hizo kuvamiwa, au wengine kutumia password moja kwenye account zaidi ya moja ikiwemo email, simu na mitandao ya kijamii.