Friday 19 December 2014

DIAMOND APEWA ULINZI KUTOKA JESHI LA UGANDA- UPDF



 Mlinzi kutoka jeshi la Uganda 

        

VIDEO YA MWANA KUTOKA LEO KUONEKANA KWENYE VITUO VIFUATAVYO

Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’itaanza kuonyeshwa ijumaa ya 19 Decemba 2014. Ali Kiba amethibitisha kuwa video imekamilika kwa kutoa kionjo cha video hio na kusema ‘Videoimetayarishwa na muongozaji kutoka Afrika Kusini na imefanyika maeneo ya mjii wa Cape Town” .  

UTATA KIFO CHA AISHA MADINDA HUU HAPA


MENGINE yameibuka! Kifo cha aliyekuwa mnenguaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ kimeibua mengine ambapo baadhi ya watu wa karibu wanaamini kimetokana na kudungwa sindano tano za majimaji yenye madawa ya kulevya, ‘unga’ na rafiki yake, Ijumaa ‘Kubwa’ linakupa zaidi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Aisha alidungwa kwa makusudi sindano hizo na rafiki yake mmoja ambaye polisi bado wanamtafuta, ikidaiwa lengo lilikuwa kummaliza.

MJUE AISHA MADINDA KUANZIA KIGOMA,UHOLANZI,DUBAI,DAR HADI UMAUTI....

 
Aisha Madinda Enziza uhai wake.

Amekwenda mapema mno! Siku ya Desemba 17, mwaka huu haikuwa poa hata kidogo kwenye tasnia ya muziki wa dansi Bongo katika kipengele cha unenguaji.Chumba chetu cha habari  kinachofanya kazi kwa karibu na mastaa Bongo kilipata mshtuko wa aina yake.
Zilikuwa ni habari mbaya za kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ inayosimamiwa na Kampuni ya ASET chini ya mkurugenzi wake, Asha Baraka, Mwanaisha Mohamed Mbegu. Wengi tulimzoea kwa jina la stejini la Aisha Madinda. 

NDOA NDOANO: MCHEKI MAIMARTHA ALIVYOZEEKA


Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ ameibuka na kusema kuwa kitendo cha yeye kuingia kwenye maisha ya ndoa kimemsababisha sasa aonekane kama aliyezeeka kwani mambo mengi ya kisichana ameyaacha. 

THEY CHEAT AGAIN....DIAMOND ANYAKUA TUZO NYINGINE

 

VAN VICKER AWASHANGAA WABONGO

                                             
Mwigizaji na mwongozaji wa filamu wa nchini Ghana, Van Vicker ameshangazwa na vyombo vya habari za udaku za hapa Bongo, kwa kile ambacho kimelipotiwa kuhusu yeye na muigizaji Wema Sepetu.
Kwenye blogs na magazeti mbalimbali ya udaku hapa Bongo zilijaa habari za kuwa Wema na Van Vicker mbali kucheza movie kuna mambo mambo walifanya eti kwa sababu tu Wema ameachana na aliekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz na hivyo alitaka kumrusha roho, kitu ambacho hakina ukweli wowote. 

Thursday 18 December 2014

WAZIRI ANNA TIBAIJUKA ASEMA AKIJIUZURU RAIS ATAMSHANGAA...

 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka amegoma kujiuzulu kwakuwa haoni sababu ya kufanya hivyo...