Wednesday 10 December 2014

WOLPER AACHANA NA MAMBO YA ANASA AWAKUMBUKA WAZEE....



Staa wa filamu Bongo Jacqueline Wolper Massawe akisalimiana na Sista wa Kanisa Katoliki la Msimbazi, jijini Dar.

STAA Jacqueline Wolper Massawe, ambaye ni muigizaji mahiri wa filamu, amewapiku nyota wenzake wa tasnia hiyo baada ya kufanya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jumamosi iliyopita kwa namna tofauti kabisa, kwani badala ya kuita marafiki kwenye pati kubwa inayoambatana na vyakula na vinywaji, yeye alikwenda kuwatembelea wazee wanaolelewa katika Kanisa Katoliki la Msimbazi, jijini Dar. 

WEMA SEPETU NOMA....AAMUA KUMFUATA VAN VICKER WA GHANA


KIMENUKA TENA HUKO KILOSA,BARABARA DAR-DOM YAFUNGWA MASAA MAWILI

WATU kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea jioni ya jana huko Dumila mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo polisi wameingilia kati na kutumia mabaomu ya machozi kutuliza ghasia hizo. 

MATOKEO UEFA HAYA HAPA....

Michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea usiku wa jana ikiwa kwenye mzunguko wake wa mwisho wa hatua ya makundi . Katika michezo iliyopigwa jana timu ya Arsenal toka England ilifanikiwa kushinda kwenye mchezo wake dhidi ya Galatasaray ya Uturuki kwa matokeo ya 2-4 katika mchezo uliopigwa huko Istanbul. 

Tuesday 9 December 2014

WALE MAPACHA WALIOUNGANA HUKO INDIA WAPATA MPENZI..


Mapacha ambao wameungana huko Bengal Magharibi Ganga na Jamuna Mondal 45, wamesema hawajawahi kuwa na mpenzi katika maisha yao kwa sababu ya kukataliwa kutokana na mwonekano wao.
Mabinti hao ambao wanatumia mikono minne na miguu mitatu wamesema kwa sasa wanafuraha ambayo hawajawahi kuwa nayo katika maisha yao baada ya kukutana na mwanaume aliyewapenda kwa mara ya kwanza Mwalimu Jasimuddin Ahmad.