Sunday 30 November 2014

HELIKOPTA YA KUKABILIANA NA UJANGILI YAANGUKA DAR


HELIKOPTA ya Wizara ya Maliasili na Utalii, iliyotolewa msaada kwa ajili ya kupambana na majangili Juni mwaka huu, imeanguka na kuua watu wanne, waliokuwa katika helkopta hiyo wakiwemo marubani wawili wa Jeshi la Polisi, askari mmoja na rubani mwingine ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Helikopta hiyo aina ya Robertson R44 yenye thamani ya Dola za Marekani 500,000 (Sh milioni 800), ilitolewa msaada na Taasisi ya Howard Buffet kwa ajili ya kusaidia mapambano hayo.

Ajali ya helikopta hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), ilitokea jana saa 4:00 asubuhi maeneo ya Kipunguni B, Moshi Bar, wilayani Ilala, wakati ilipokuwa katika ukaguzi wa kawaida.

MKULIMA APIGWA RISASI NA POLISI BAADA YA KUVAMIA KITUO HUKO SINGIDA


MKULIMA mkazi wa kijiji cha Mitundu tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,Esther Salumba (30) amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi wakati wa vurugu za kuvamia kituo kidogo cha polisi kilichopo kijijini hapo.