Friday 28 November 2014
WAZIRI Prof MUHONGO ASEMA FEDHA ZA ESCROW SI MALI YA UMMA,ADAI BADO SERIKALISERIKALI INADAIWA..
Akiwasilisha maelezo ya Serikali leo, Prof Muhongo alipangua hoja moja baada ya nyingine zilizotolewa na Kamati ya PAC jana na kusisitiza kuwa fedha hizo si mali ya umma.
Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow linaendelea kuchukua sura mpya baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutoa ufafanuzi wa Serikali bungeni mjini Dodoma kuwa fedha hizo si za umma na kwamba bado Serikali ina mzigo wa madeni katika sakata hilo.
Kauli ya Prof Muhongo inakuja siku moja baada ya Kamati ya PAC kuwasilisha ripoti yake jana juu ya suala hilo ambapo pamoja na mambo mengine, Kamati ya PAC ilijiridhisha kuwa sehemu ya fedha hizo ni za Serikali.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akisoma taarifa ya kamati hiyo jana alisema Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Francis Mwakapalila, Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade wakithibitisha kuwa sehemu ya fedha zilizokuwamo kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa za Serikali.
Akiwasilisha maelezo ya Serikali leo, Prof Muhongo alipangua hoja moja baada ya nyingine zilizotolewa na Kamati ya PAC jana na kusisitiza kuwa fedha hizo si mali ya umma.
Prof Muhongo pia alitumia muda mwingi kueleza jinsi Kampuni ya uwakili ya Mkono and Advocates iliyokuwa ikiitetea Serikali pamoja na Tanesco, ilivyochota kiasi kikubwa cha pesa kama malipo ya kazi hiyo tangu kuanza kwa mgogoro huo.
“Gharama za mawakili; Kampuni ya Mkono & Advocates waliokuwa wakiitetea Tanesco na Serikali katika suala la IPTL tangu mwaka 1998 hadi 2013 ni Sh62.90 bilioni na bado wanaidai Serikali $ milioni nne,” alismea Prof Muhongo.
Aliongeza kuwa Kampuni hiyo ya Mkono & Advocates iliishauri Serikali kuwapa kazi nyingine ya kwenda kuitetea Serikali juu ya mgogoro huo, lakini Serikali ilikataa na kuongeza kuwa waliokoa Sh95 bilioni kwa uamuzi huo kwani uwezekano wa kushinda ulikuwa mdogo.
DIAMOND NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA
Hii ni mara ya pili kwa msanii Diamond Platnumz kualikwa ndani ya jumba la BBA akiwa na mwanamuziki kutoka Congo, Fally Ipupa ambapo wameshiriki chakula cha mchana pamoja na washiriki waliobaki kwenye Jumba hilo, safari hii wasanii hao wameingia kwa ajili ya kuhamasisha ONE Campain ambayo inahusu kilimo, moja ya Project zilizowahi kufanywa na Kampeni hiyo ni ile nyimbo ya Cocoa na Chocolate ambayo wameshiriki pia mastaa wengine kibao kutoka Afrika.
KOCHA WA CHELSEA APEWA KAZI KUINOA GHANA
Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Avram Grant ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Ghana.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 alitia saini kandarasi ya kufunza kwa miezi 27 na kuchukua uongozi kutoka kwa Maxwell Konadu, ambaye amekuwa kocha wa muda tangu Kwesi Appiah alipoondoka mwezi wa Septemba.
Ataanza kazi Jumatatu na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa Februari 2017 - baada ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Raia huyo wa Israeli ana wiki sita tu kuiandaa Black Stars kwa ajili ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Equatorial Guinea.
Shirikisho la kandanda nchini Ghana limetoa ruzuku kwake kwa "kufanya vizuri" katika mashindano hayo na amepewa muda mfupi na timu hiyo na kuwa atashinda kombe hilo miaka miwili ijayo.
Ghana, ambayo iliongoza katika kufuzu kwenye kundi lao ili kushiriki mashindana hayo mwaka ujao, itapata kujua wapinzani wao nchini Equatorial Guinea wakati droo itakapofanywa tarehe 3 Desemba.
Mashindano yatafanyika kati ya Januari 17 na 8 Februari.
Grant, ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Chelsea alishindwa na Manchester United katika fainali za mwaka wa 2008 katika Ligi ya Mabingwa, alipohudumu hadi hivi majuzi ambapo alichaguliwa kuwa mkurugenzi wa kiufundi katika klabu ya BEC Tero Sasana nchini Tahailand.
Jukumu lake la mwisho kama kocha lilikuwa katika klabu ya Partizan Belgrade kati ya mwaka 2012-2014, wakati ambapo aliongoza klabu hio kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya tano.
Kando ya kuviongoza vilabu vya Uingereza vya Portsmouth na West Ham, Grant ana uzoefu wa kimataifa kwani aliifunza timu ya taifa ya Israeli kwa miaka minne.
Kumekuwa na wale wamekuwa na wasiwasi kwamba utaifa wa Grant ungeweza kumzuia kuingia baadhi ya nchi za Afrika Kaskazini.
Rais wa shirikisho la kandanda nchini Ghana, Kwesi Nyantekyie aliiambia BBC Michezo "kwamba ni suala" lakini anasema kuwa pande hizo mbili zitakabiliana nalo.
"Mmiliki wa pasipoti ya nchi ya Israel hatakataliwa tu kuingia nchi za Afrika Kaskazini,bali pia atazuiliwa kuingia baadhi ya nchi za Kiarabu," alisema.
"Yeye ameleta njia mbadala ya kukabiliana nayo. Kuna utaratibu wa kuridhisha wa kukabiliana na tishio lake.
Hivi karibuni, katika miezi michache ijayo, tutashughulikia kikamilifu mambo hayo."
CHANZO: BBC
BI HARUSI AMLISHA MUMEWE SUMU
Bi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake.
Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu.
Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa.
Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho.
Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri.
Msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi'u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5 mwezi Aprili,siku ambayo bwana Sani alifariki.
''Alisema kuwa panya wanamsumbua katika chumba chake'',Hamziyya aliiambia mahakama.Upande wa mashtaka baadaye ulisema kuwa badala yake Tas'u aliweka sumu hiyo ya panya katika chakula ambacho alikuwa amekiandaa kwa sherehe za baada ya harusi kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa bwana Sani.
Msichana huyo alikataa kuzungumza mahakamani.
Jaji Mohammed Yahaya,katika mahakama ya Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u ambaye alikataa kuongea katika mahakama hana hatia katika kusikizwa kwa kesi mnamo mwezi Octoba ambapo alisomewa mashtaka.
Jaji huyo alikataa ombi la upande wa mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama ya watoto.
Ushahidi wa Hamziyya uliungwa mkono na Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza sumu hiyo kwa mtoto huyo.
Jirani ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim Ibrahim alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba alipewa chakula hicho kilichopikwa na Tasiu.''Nilipoletewa chakula hicho niliona vipande vipande vyeusi''aliiambia mahakama.
Alikula vipande vinne vya madonge vilivyotengezwa na maharagwe lakini hakupendelea ladha yake'',alisema na kuongezea kuwa ni Umar pekee aliyeendelea kula.
Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka nyumbani.
Lakini alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana sani ,aligundua kwamba watu wengine watatu ambao walikuwa wamekula chakula hicho wamefariki kwa ghafla.
Viongozi wa mashtaka walidai kwamba chakula cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua watu wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao katika kesi moja ya mauaji.
Nigeria haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya uhalifu tangu mwaka 1997,ambapo taifa hilo liliongozwa na dikteta Sani Abacha,kulingana na shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch.
CHANZO: BBC
CHANZO: BBC
SHEIKH PONDA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA KUU
Mahakama Kuu ya Tanzania imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda baada ya kuona hana hatia dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self iliyokuwa inamkabili.
Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema baada ya kupitia vifungu vyote mahakama imejiridhisha na kuona Sheikh Ponda hana hatia yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa rumande akisubiri kesi nyingine ya madai ya uchochezi, Mkoani Morogoro inayomkabili.
Thursday 27 November 2014
MAITI ZA WALIOKUFA KWA EBOLA ZATUPWA HOVYO MTAANI
Wahudumu wa Afya nchini Sierra Leone waliopewa kazi ya kuzika maiti za wagonjwa waliokufa kwa ebola wameamua kuitupa miili hiyo mitaani kutokana na kulalamikia posho ndogo wanazolipwa na Serikali ya nchi hiyo.
Katika kitendo cha kushangaza waliamua kutupa miili 15 ya maiti hizo katika mitaa mbalimbali kwa lengo la kuelezea hisia zao za kuchoshwa na malipo madogo wakati wanafanya kazi kubwa.
Wafanyakazi hao waliripotiwa kukaa siku saba bila kulipwa fedha zao ambapo kwa wiki hulipwa dola100 ambazo walidai ni ndogo ukilinganisha na kazi waliyokua wakifanya kudai inahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa.
Nyongeza ya fedha hizo walizokua wakitaka ni kwa ajili ya kufidia kazi wanazofanya kwa sababu hufanya katika mazingira magumu ya kuzika wagonjwa wa Ebola ambao huambikizwa kwa njia ya kugusana.
Kituo cha kitaifa kinachosimamia ugonjwa wa Ebola nchini humo kilitangaza rasmi kuwa wafanyakazi wote walioshiriki katika mgomo huo watafukuzwa kazi.
EMERSON AANZA MAZOEZI YANGA
Emerson de Oliveira Neves Roque – mbrazil ambaye ameletwa nchini kuja kufanya majaribio na endapo ikifuzu basi ndio itachukua nafasi ya mbrazil aliyeondoka Jaja.Jana jioni mchezaji huyo huyo aliwasili na leo hii mchezaji huyo ameanza mazoezi mepesi asubuhi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola kufuatia kusaifri kwa zaidi ya masaa 11 kutoka jijini Rio de Janeiro.
Kiungo mbarazil Emerson de Oliveira a(wa pili kutoka kulia) akiwa mazoezini leo asubuhi katika uwnaja wa shule ya sekondari Loyola, wengine ni Kizza, Javu na Coutinho
Emerson ameungana na wachezaji wengine wa Young Africans katika mazoezi ya leo asubuhi ikiwa ni siku yake ya kwanza katika ardhi ya Tanzania na kufanya mazoezi mepesi mepesi chini ya kocha msaidizi Leonardo Neiva kuijiweka fit na kutoa uchovu safari.
Kiungo huyo mwenye umbo lililonyumbulika ambae alikuwa akichezea timu ya Bonsucesso FC iliyopo lii daraja la pili nchini Brazi katika jiji la Rio de Janeiro pia msimu uliopita alikua akicheza soka la kulipwa katika nchi ya Poland latika klabu ya Piotrkow Trybunalski FC.
Kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo amesema mchezaji huyo leo alikua na programu ya mazoezi mepesi tu kutokana na uchovu wa safari na kesho anatarajiwa kuendelea na mazoezi na wenzake kulingana na ratiba iliyopo.
Endapo Emerson atafanikiwa kulishawishi benchi la Ufundi kumsajili basi moja kwa moja ataingia makubaliano na klabu ya Young Africans kwa ajili ya kuitumikia kwenye michuano ya kimataifa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia bara.
HAYA NDIO MAJIBU ALIYOYATOA Mh MIZENGO PINDA BUNGENI MAPEMA LEO ASUBUHI
Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata vilema…“– Mbowe.
"Tumeona mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
"Baada ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio fedha za umma?“– Mbowe.
"Kwa uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…“
"Ningeweza nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Subscribe to:
Posts (Atom)