Thursday 27 November 2014

KASHFA YA MISS TANZANIA 2014,UTATA MPYAAAAAAA WAIBUKA


Hatima ya kashfa ya kudanganya umri inayomkabili aliyekuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2014, Sitti Mtemvu bado ipo kizani baada ya polisi kuikana kauli ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

Rita, kwa upande wao ilieleza wiki moja iliyopita kuwa imekabidhi polisi vielelezo kuhusu uchunguzi wa kashfa hiyo kwa lengo la kuchukua hatua.

Juzi, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikana kupokea taarifa za vielelezo hivyo vilivyotumiwa kuombea cheti cha kuzaliwa cha Sitti Mtemvu.

Wiki mbili zilizopita, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ilijivua lawama katika kashfa hiyo na kuiachia Rita.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Kova alisema, “Jeshi la Polisi halijapokea vielelezo vyovyote kutoka Rita, wamepeleka wapi? Iwapo waliviwasilisha katika kituo chochote cha polisi watoe taarifa iliyo sahihi, iwapo vielelezo hivyo vitatufikia tutachukua hatua stahiki,” alisema Kova.

Kwa upande wao, Rita waliahidi kuwasilisha vielelezo hivyo wiki hii na kwamba vilicheleweshwa kutokana na kukamilisha upekuzi wa taarifa za kuombea cheti pamoja na cheti cha awali kilichokuwa kikitumiwa na Sitti Mtemvu.

Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Rita, Emmy Harrison alisema jana kuwa idara yake imekamilisha taratibu zote zinazotakiwa na vielelezo hivyo vitakabidhiwa rasmi polisi.

“Haya ni masuala ya kisheria, hivyo sisi tumeshakamilisha kile tulichotakiwa kukifanya na mchakato huu bado unaendelea, tupo katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kuripoti polisi, wiki hii vielelezo vya Sitti vitapelekwa kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema Harrison.
CHANZO: MWANANCHI

MRITHI WA JAJA HUYOOOOOOOOO KASHATUA.......



Nyota mpya wa Klabu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam, anayekuja kufanya majaribio ya kuziba nafasi ya Mbrazil mwenzake Genlson Santos 'Jaja', Emerson De Oliveria Neves Rouqe akitoa ishara ya dole mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa Yanga. 
Rouque aliwasili na Kocha mkuu wa Yanga, Marcio Maximo pamoja na Nyota mwingine kutoka Brazili Andrew Coutinho.

ICHEKI SURA YA YULE BEKI TATU WA UGANDA BAADA YA KUPOKEA KICHAPO HEVI



Huu ndio muonekano wa yule msichana wa kazi za ndani aliye tenda unyama wa kutaka kumuua mtoto wa bosi wake atimaye naye amepokea kipigo takatifu cha nusu kufa kutoka kwa wazazi wa uyo mtoto hii ni moja ya picha zilizo vuja ambazo wazazi wa mtoto family iyo walizificha.

VYUO VIKUU TANZANIA HOVYO KABISA....VYAIAIBISHA NCHI...


Vyuo vikuu vitatu vya Tanzania ambavyo vilishiriki katika mashindano ya mjadala wa Afrika kuhusu Sheria za kimataifa za haki za kibinaadamu yalioandaliwa na kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC vimeshindwa kufika katika raundi ya mwisho.

Badala yake vyuo hivyo viliondolewa katika raundi za mapema ambapo mataifa manane ya Afrika yalishiriki.

ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa mjini Arusha.

Kulingana na gazeti la the Citizen nchini Tanzania, vyuo vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo kikuu cha Zanzibar.

Katika raundi ya mwisho ya mashindano hayo yaliofanyika mwishoni mwa wiki katika mahakama maalum ya kimataifa inayochunguza mauaji ya kimbari nchini Rwanda ICTR mjini Arusha,chuo cha Strathmore University kutoka Kenya kiliibuka mshindi na kufuatiwa na chuo cha Christian University kutoka Uganda huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka Zimbabwe kikiibuka mshindi wa spika bora.

Raundi ya mwisho ya mjadala huo ilisimamiwa na jaji wa mahakama hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji wa mahakama ya haki katika Afrika mashariki Fanstin Ntezilyayo,John Joseph Wamwara na Mutsa mangezi kutoka ICRC.

Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi kwa washindi aliyapongeza mashindano hayo kama kifaa cha kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya sheria na kwamba itasaidia kuimarisha maono yao katika siku za usoni.

UBAGUZI WA RANGI WAKITA MIZIZI MAREKANI....WATU WEUSI WAWEKWA GEREZANI,WAHUKUMIWA KIFO NA WENGINE WAPIGWA RISASI NA POLISI


Mkuu wa Haki za Binaadamu Katika Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu 'ubaguzi uliokita mizizi' na idadi kubwa kupita kiasi ya Wamarekani weusi au wenye asili ya Afrika ambao wanauawa na polisi nchini Marekani.

Zeid Ra’ad Al Hussein Kamishna wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa kuna idadi kubwa kupita kiasi ya Wamarekani weusi wanaoshikiliwa gerezani na wanaosubiri kutekelezwa hukumu za kifo dhidi yao.

Matamshi hayo yametolewa kufuatia ghasia kubwa zilizoibuka baada ya jopo la mahakama huko Missouri, Marekani kumuondoa hatiani afisa mzungu wa kikosi cha polisi ambaye alimpiga risasi na kumuua kijana Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Michael Brown, katika mji wa Ferguson. Ghasia zimeripotiwa katika miji zaidi ya 90 kote Marekani ambapo waandamanaji wanalalamikia ukandamizaji na ubaguzi wa wazi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika katika mfumo wa utawala nchini Marekani. Gavana wa Jimbo la Missouri, Jay Nixon, ameagiza wanajeshi wengine 2,200 wa Gadi ya Taifa kupelekwa Ferguson kukabiliana na waandamanaji wenye hasira.

MTI ULIOINUKA BAADA YA KUANGUKA MIAKA 3 ILIYOPITA WAENDELEA KUFANYA MAAJABU


Mti huo umeinuka siku ya Oktoba 15 mwaka huu, ambapo Katibu tawala wa Wilaya ya Uyuwi amesema;
 “…kwa mazingira tunayoyaona hapa tukio ni kweli limetokea sasa ni kwa nguvu zipi kwa uwezo wa Mungu au nguvu za giza hili nadhani kwa sasa litakuwa hatuwezi kulitolea taarifa ,lakini cha msingi eneo hili tulitunze kwa matumizi ya kumbumbuku ya vizazi vyetu na pamoja na wengine watakaotoka nje ya eneo hili, ambao watataka kuja kuona maajabu ya Mwenyezi Mungu tofauti na kule Mfuto ulipoinuka tu siku ya pili yake tukakuta kila kitu hakuna, kwa hiyo nilikuwa napenda niwapongeze Wanakijiji kwa kulinda Mti huu…”

Shuhuda wa kwanza kuzungumzia tukio hilo amesema; “… Haya magome ya mzizi yakichimbwa, yakisagwa mtoto akiwa anaumwa Degedege wakimvutisha ile hali ya mchango inashuka hata kama unaumwa kipanda uso, hata kama unaumwa kichwa cha kawaida…”

Mwanakijiji mwingine amesema; “…Huu Mti kama mbwa wako sio mkali unachimba mizizi unakoboa magome unatwanga ule unga wake unamnusisha kwenye pua anakuwa mkali sana…“

Mtu mwingine amesema; “Kama kuna Mtu ambaye pengine kashaishiwa pengine fahamu wanajaribu kumuwekea puani na mara anapiga chafya…”

Mh MKONO HAKULISHWA SUMU


         Mh.Nimrod Mkono (MB).

Siku chache baada ya Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London Uingereza,Mbunge wa Chadema Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.
Mkono alisema leng la kulishwa sumu ni kutaka kuharibu figo zake ndani ya saa72 lakini kitendo hicho kilichoshindikana.
Mdee aliyekua na Mkono katika ziara hiyo nchini Uingereza alisema hakuna ukweli wowote kuhusu yeye kutaka kulishwa sumu,nilikua naye kule na mazingira ya kuanza kuumwa hadi kupona kwake ni utata mtupu….awaeleze Watanzania anaumwa nini na si kusingizia alilishwa sumu,”alisema.
‘Kama anataka kutumia kivuli cha Escrow,arudi bungeni tuweze kujadili na tuimalize ili asiseme kuwa sijui wanataka kumuua ni uongo.

RICK ROSS APATA DEMU MPYAAAAAAAA BONGE LA TAJIRI....



Rick Ross The Boss ambaye aliwahi kuja Tanzania kwenye Fiesta, juzi kati alifanya party ya kusherehekea album yake mpya ya Hood Billionaire huko Atlanta Georgia Marekani.
Unaambiwa kwenye party hiyo Rozay alikua bega kwa bega na mrembo Ming Lee ambaye anatajwa kuwa milionea kutokana na biashara ya nywele na kampuni yake ambayo inahusisha pia nguo na Salon.
Baada ya kuonekana pamoja zimeanza kusambaa fununu kwamba Rozay ndio kajiegesha hapo kwa sasa.