Saturday 22 November 2014

RATIBA YA LIGI KUU UINGEREZA LEO HII


Chelsea v West Brom18:00

Everton v West Ham18:00

Leicester v Sunderland18:00

Man City v Swansea18:00

Newcastle v QPR18:00

Stoke v Burnley 18:00

Arsenaly v Man Utd 20:30

Mechi zote kuchezwa saa za Afrika Mashariki

Friday 21 November 2014

RONALDO AOSHA VYOMBO BAADA YA KUSHINDWA KAMARI


Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikabiliana vilivyo na mwana tenisi huyo kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili hao katika meza ya pokerstar, Casino ya Hippodrome mjini London ambapo Nadal alishinda fedha hizo.

Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.

Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula.

MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI DUNIANI 2014 KITAIFA KUFANYIKA NJOMBE


Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani kwa mwaka 2014 kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Njombe kuanzia tarehe 24 mwezi huu hadi tarehe  moja  Desemba.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya tume hiyo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mrisho alisema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tanzania bila maambukizo mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), Vifo vitokanavyo na UKIMWI, Ubaguzi na unyanyapaa inawezekana.

“Kauli mbiu hii inalenga kutoa msukumo wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kudhibiti UKIMWI kitaifa na kimataifa ili kufikia azma ya sifuri tatu zinazomaanisha maambukizi mapya sifuri, vifo vitokanavyo na UKIMWI sifuri na unyanyapaa sifuri ifikapo mwaka 2018”.


Kauli mbiu hii pia inahimiza utekelezaji wa dhati wa malengo ya Maendeleo ya Milenia na maazimio yaliyowekwa kwenye mkutano maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI uliofanyika mwaka 2001 nchini Marekani”, alisema Dkt. Mrisho.

Alisema kipaumbele cha maadhimisho ya mwaka huu ni upimaji wa hiari wa VVU na ushauri nasaha, na kutoa  wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma hii muhimu.

Aidha Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi kuadhimisha siku hiyo kwa njia ya makongamano, kumbukumbu za waliofariki kwa UKIMWI, midahalo, mikutano ya wazi, vipindi kupitia vyombo vya habari, kutembelea na kutoa misaada kwa watoto yatima na wanaougua ugonjwa huo  na kutoa elimu inayohusu kujikinga na maambukizi.


Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa TACAIDS Dkt. Raphael Kalinga alisema dawa hizo hutolewa  bila malipo kwa wahitaji wanaostahili kuzipata hii ni kulingana na mfumo wa utoaji kwa wahitaji.

“Kuna baadhi ya wagonjwa hulazimisha kupewa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI ingawa kinga zao bado zinamudu kukabiliana na tatizo hilo wakati si sahihi kufanya hivyo. Kwani wanaostahili kupata dawa hizo ni wale ambao kinga zao zipo  chini”, alisema  Dkt. Kalinga.

Maadhimisho ya wiki hiyo yataenda sambamba na maonyesho ya shughuli za wadau wa udhibiti UKIMWI nchini na kongamano la kitaifa la kutathimini hali  na mwelekeo wa udhibiti  wa ugonjwa huo.  


11 WAPOTEZA MAISHA KANISANI

Polisi ya Zimbabwe imetangaza kuwa kwa watu 11 wamepoteza maisha kutokana na msongamano mkubwa wa watu, wakati walipokuwa wakitoka katika uwanja mmoja baada ya kumaliza ibada ya Kikristo. Shadreck Mubaiwa, Msemaji wa Polisi ya nchi hiyo amesema kuwa, watu wanne walifariki katika eneo la tukio huku wengine saba wakipoteza maisha hospitali. Ameongeza kuwa, mauaji hayo yalitokea jana usiku katika mji wenye kuchimbwa madini wa Kwekwe, yapata kilometa 220 kutoka Harare, mji mkuu wa Zimbabwe wakati idadi kubwa ya watu walipokuwa wakitoka katika uwanja wa mji huo kwa ajili ya ibada. Watu wengine wamejeruhiwa na wengine hali zao zikiwa mahututi. Inaelezwa kuwa, maelfu ya watu walikuwa wamehudhuria katika ibada hiyo iliyomalizika majira ya usiku.

23 WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI SINGIDA


JESHI la polisi mkoa wa Singida, linawashikilia watu 23 wakazi  wa kijiji cha Nkyala kata ya shelui wilaya Iramba mkoa wa Singida, kwa tuhuma ya kudaiwa kuuawa kwa makusudi wezi wanne wa madume ya Ng’ombe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka, alisema watu hao kati yao 21 wanatuhumiwa kwa mauaji na wawili wanatuhumiwa kuiba ng’ombe watatu.

Aliwataja watu hao waliouawa kwa tuhuma ya wizi wa madume matatu ya ng’ombe ni Magupa Ngelela (32), Hemedi Masasi (29), wote wawili ni wakazi wa kijiji cha Nkyala.Wengine ni Saidi Hamisi (32) mkazi wa kijiji cha Kinkungu na Didas Mwigulu (36) mkazi wa kijiji cha Mgongo.

Akifafanua,alisema novemba 19 mwaka huu saa saba usiku,watu hao wanne kwa pamoja inadaiwa walivunja zizi la Omari Iddi mkazi wa kijiji cha Nselembwe na kuiba madume matatu ya ng’ombe.

Alisema asubuhi yake,watu hao walifumwa wakiwa tayari wameisha wachinja Ng’ombe hao na bila kuwachuna,waliwakata kata na kujaza nyama kwenye mifuko ya sadarusi.

“Walivamiwa na kuanza kupigwa kwa silaha za jadi na walipofariki dunia,walichomwa moto”,alisema.

Alisema uchunguzi ukikamilika,watu watakaobainika kuhusu na mauaji hayo ya kikatili,watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili ya mauaji na wizi wa Ng’ombe.

“Kwa sasa hatuwezi kutangaza hadharani majina ya watuhumiwa tunaoendelea kuwashikilia, kwa vile kitendo hicho kinaweza kuharibu kazi ya upelelezi ambao bado unaendelea”, alisema kamanda Sedoyeka.

MH SITTA AMTETEA SHY ROSE BHANJI



Kumekuwa na taarifa kuhusu kuwepo migogoro mbalimbali inayohusisha Wabunge wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo Mbunge Shy-Rose Bhanji amehusishwa sana kwenye vichwa vya habari.

Kwenye kikao cha Bunge November 20 2014 Dodoma Hatibu ambae ni mbunge wa Zanzibar aliuliza ,"Sisi wabunge wa bunge hili ndiyo wapiga kura wa kuwachagua wawakilishi wetu wa kutuwakilisha katika bunge la Afrika Mashariki, kumekuwa na taarifa za kulipaka Taifa hili matope kulitia aibu kutokana na  baadhi ya wawakilishi wetu, Wabunge wetu wa Afrika Mashariki kutokana na matendo wanayoyafanya kule..”

“…Ni lini hasa kinachoendelea pale na hatua gani zilizochukuliwa kuhusu ukosefu wa nidhamu uliojitokeza kwa mbunge Shyrose Banji wazi wazi na ili hali hakuna taarifa yoyote, Mheshimiwa Naibu Spika naomba mwongozo wako…”– Hatibu.

Baada ya swali waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akawasha kipaza sauti na kutoa haya majibu “…Naomba nitoe taarifa kwamba kinachotokea katika Bunge la Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa kinahusu mgogoro wa  spika mwenyewe, hilo ndiyo chanzo cha matatizo mengi, kwa hiyo  wabunge  wa Bunge la  Afrika Mashariki wamegawika kataka makundi mawili, kuna kundi linalotaka Spika lazma aondolewe, na wengine wanadai wanamtetea abaki…”
..Sasa katika kundi ambalo wanataka  abaki imeonekana Tanzania ndio kikwazo, kwa sababu ili upate uamuzi ndani la Bunge la Afrika Mashariki  katika suala lolote lazima upate akidi inayotosheleza kutoka  kila nchi, sasa wabunge wa Tanzania ambao mwanzoni waliunga mkono hoja ya kumuondoa yule Spika wamefuta hilo na wamekubaliana aendelee kwa hiyo imeleta chuku kiasi Fulani…“– Sitta.
 “…Katika tukio ambalo limetokea juzi nasema hivi kwa sababu  Naibu Waziri wangu yuko kule kwa hiyo ni jambo halisi, kilichotokea sio kama kinavyoelezwa Mheshimiwa Shyrose Banji ambaye anahesabika ni mfuasi mkubwa wa Yule Spika kiasi kwamba wenzie wanamuona kama kibaraka vile, alikuwa anapita katikati ya Wabunge wengine kuwahi usafiri kwa bahati mbaya akamgonga Mheshimiwa Ndelakindo Kessy, Mheshimiwa Ndelakindo akahamaki na kwa kusaidiwa na  baadhi ya Wabunge  wengine wa Uganda akaenda kituo cha Polisi kutoa taarifa kwa madai kwamba amefanyiwa makosa ya jinai wanaita ‘assaults’…“– Sitta.

Ikabidi aitwe ‘Sergeant at Arms’ wa Bunge la EALA ambaye alikwishaanza jitihada za kulifanya jambo lile liishie ndani ya Bunge na katika jitihada hizo alifika mbali kidogo akawezesha Wabunge wetu hao wawili waweze kusikilizana na ninavyotoa taarifa hivi sasa ni kwamba jana suala hili limekwisha na haliendelezwi na Polisi tena…
“– Sitta.Hivi ndivyo Waziri Sitta alimalizia kujibu suala hilo;

Sasa yale mengine yaliyosema kwamba alifanya mambo ya hovyo Mheshimiwa yule tena kama miezi miwili iliyopita, bado yako mikononi mwa tume ya Bunge la Afrika Mashariki hadi hapo watakapolishughulikia hatuwezi kufanya kitu chochote, na tukishapata taarifa ya tume ya Bunge la Afrika Mashariki basi mimi nitatoa taarifa kwa Mheshimiwa Spika ili sasa sisi kwa wote kama jimbo la uchaguzi La Wabunge hao tuone ukweli ni upi na tujue hatua ya kuchukua..”– Sitta.

MAGAZETI YA UDAKU NA MICHEZO










MAGAZETI YA KIBONGO LEO HII





8